Tema yaliyo moyoni,
Sema nami kilicho rohoni,
Nena yasijejaa hadi pomoni,
Yakakuziba na kukaba kooni.
Uamkapo livalie tabasamu usoni,
Utembeapo tafakari hili fikirani,
Tia bidii ndo unoge kwa fani,
Upate raha ukabarizi jioni.
Yachague kwa makini yako maneno,
Kwani yana ncha mbili kama msumeno,
Yawe ya kufaa na kupigiwa mfano,
Upate furaha kupitia kila vuno.
Ninaposema nisikize kwa makini,
Ninapotema nielewe ewe mwandani,
Haya maisha ni ya ajabu iso kifani,
Yachangamsha na kustaajabisha bila utani.
© Patolyer 2013
Sema nami kilicho rohoni,
Nena yasijejaa hadi pomoni,
Yakakuziba na kukaba kooni.
Uamkapo livalie tabasamu usoni,
Utembeapo tafakari hili fikirani,
Tia bidii ndo unoge kwa fani,
Upate raha ukabarizi jioni.
Yachague kwa makini yako maneno,
Kwani yana ncha mbili kama msumeno,
Yawe ya kufaa na kupigiwa mfano,
Upate furaha kupitia kila vuno.
Ninaposema nisikize kwa makini,
Ninapotema nielewe ewe mwandani,
Haya maisha ni ya ajabu iso kifani,
Yachangamsha na kustaajabisha bila utani.
© Patolyer 2013
Comments
Post a Comment